Uongozi wa SIMBA Wawaangukia Wachezaji, Ishu iko Hivi

Uongozi wa SIMBA Wawaangukia Wachezaji, Ishu iko Hivi

Uongozi wa Simba SC umewataka Wachezaji wa Klabu hiyo kupambana na kutambua uchungu wanaoupata Mashabiki na Wanachama pale mambo yanapokwenda mrama.


Ombi hilo kwa Wachezaji wa Simba SC limewekwa hadharani kufuatia mambo kuwaendea mrama wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans, uliomalizika kwa Mnyama kupigwa 5-1, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Novemba 05.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema wachezaji wanapaswa kutambua hilo na kuhakikisha wanapambana vilivyo katika kila mchezo ili kufanikisha furaha kwa Mashabiki na Wanachama ambao wamekuwa bega kwa bega na timu yao.

“Wachezaji sisi tuna imani nao, tarehe 25 wakaendeleze makubwa. Waamke sasa wakaipiganie Simba. Wanayo kazi kubwa ya kutufutia hizi kejeli kwa wao kufanya vizuri. Tukipata matokeo mazuri watapunguza machungu makubwa tunayopita hivi sasa.”

“Ni muhimu wajue pale hawachezi tu kwa ajili yao bali kwa ajili ya Simba. Sisi tutaenda kutimiza wajibu wa kushangilia, na wao watupe furaha ili turejeshe hali yetu ya kutamba. Tunawambia hivyo kwa niaba ya mgeni rasmi, mashabiki wa Simba.” amesema Ahmed Ally

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.