Try Again afungukia ishu ya kumshusha Sven Simba

Try Again afungukia ishu ya kumshusha Sven Simba
 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salum Abdallah 'Try Again' ameulizwa kuhusu uwezekano wa kumrejesha aliyekuwa kocha wao, Sven Vandenbroeck na ametoa majibu.

Try Again amefungukia ishu hiyo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Azam TV kuelezea mikakati yao ya kuelekea kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Novemba 25, 2023 ambapo Simba atakutana na ASEC Mimosas.

Alipoulizwa kuhusu mtazamo wa mashabiki kuona kama aliyewahi kuwa kocha wao Sven anafaa na ni mtu sahihi kwa sasa, Try Again alifunguka:

"Hayo ni mawazo ya mashabiki na sisi kama viongozi tuna mawazo yetu pia ambayo tunadhani pia...niseme tu Sven ni kocha mzuri, ni kocha ambaye amefundisha vilabu vikubwa sana sasa hivi Afrika, kwa hivyo sitaki kusema ni nani kwa sasa lakini kocha atakayekuja ni kocha bora ambaye anaifahamu vizuri Afrika," alisema Try Again.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.