Timu ya Simba Kupishana na Ubingwa Tena?

 

Timu ya Simba Kupishana na Ubingwa Tena?

Simba kutwaa ubingwa msimu huu wa 2023/24 itakuwa shughuli pevu kutokana na mwendo walionao kwenye ligi.


Novemba 5 2023 ilikuwa ni siku ya kutoa taswira ya namna bingwa atakavyopatikana na goma inaonekana Yanga wana asilimia kubwa kukomba kwa mara nyingine taji la Ligi Kuu Bara.


Ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga, wanasema ili uwe bingwa lazima umtwange yule mnayekimbizana kwenye ubingwa, kete ya pili kwa Yanga walianza na Azam FC kisha Simba.


Maxi Nzengeli alitupia mabao mawili, Aziz KI bao moja, Kennedy Musonda huyu alifungua pazia huku Pacome akifunga pazia.


Bao pekee la Simba lilifungwa na Kibu Dennis mkandaji ambaye alipata maumivu kwenye mchezo huo na kukwamakukomba dakika 90.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.