Shaffih Dauda Afunguka 'Siamini Kama Kocha wa Makipa Simba Alipendekeza Manula Adake Jana'

Shaffih Dauda Afunguka 'Siamini Kama Kocha wa Makipa Simba Alipendekeza Manula Adake Jana'


 Ameandika Haya Shaffih Dauda:

KUMEKUCHA

Baada ya mchezo wa jana kumalizika yangu ni haya nikianza na eneo la uchaguzi wa kikosi !

Kabla timu haijafikia uamuzi wa kupanga kikosi siku hizi ni tofauti na soka letu lilipotoka, siku hizi mtu ambaye anaamua nani acheze ni performance analyst hii ni kutokana na ripoti ya wiki nzima.

Yupo pia kocha wa magolikipa na wataalamu wa idara zingine, Kila mmoja atatoa ripoti kwa Kocha na wataishia hapo kwa sababu wao sio watoa maamuzi ya mwisho nani aanze kwenye kikosi

Mwalimu [Kocha Mkuu] ndio ataamua apange kwa kuangalia ripoti au apange kwa utashi wake mwenyewe lakini muda huo anakuwa tayari amepewa ripoti kutoka kwa wataalamu .

Mimi Shaffih Dauda, siamini kama kocha wa magolikipa wa Simba [Daniel Cadena] kwenye ripoti yake kuelekea mchezo wa Simba vs Yanga alimpitisha Aishi Manula kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.