Mchezaji Bacca Kazi Anayo Ashikishwa Kizizi Kutoka Zanzibar Yanga Kuia Al Ahly
Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said ameitangaza mechi ya Yanga dhidi ya Al Ahly Disemba 2/23 kuwa ni Bacca Day.
Akizungumza na Wanahabari Visiwani Zanzibar Hersi amesema walipoanza kuwapa thamani wachezaji wao walioanza kwa kuwapa siku ambao ni Max Nzengeli na Stephane Aziz Ki walipokea maoni ya wanachama na mashabiki wakiwataka wachezaji wa ndani pia kupewa siku maalum za kuwasherehekea hivyo waliyapokea na kuyafanyia kazi.
Hersi ametumia hafla hii kupongeza juhudi binafsi za Ibrahim Bacca kwa kuipambania nafasi aliyoipata klabuni hapo na amebaki kuwa bora kwenye nafasi hiyo.
Aidha katika hatua nyingine, Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema juzi taifa liliingia aibu baada ya Simba kupata sare na ASEC Mimosas na mashabiki kuingia wachache uwanjani.
Kamwe alisema, kwa kulitambua hilo, mashabiki wa Yanga watawaonesha ni namna gani uwanja unatakiwa ujae Jumamosi hii watakapokuwa wanacheza na Al Ahly katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
“CAF wasifikiri labda kuna msiba kwa kuona wameingia mashabiki 66 kwenye ule mchezo, sisi tutaujaza uwanja kurejesha heshima maana sisi ndio wenye mpira huu nchini,” alisema Kamwe.
ALSO READ:
Ligi Bora Africa | Best Football Leagues in Africa 2023/2024
ORODHA ya Vilabu Bora Afrika 2023 (CAF Club Ranking)