Mchambuzi: Simba Wapatikane Wachezaji wa Maana Tuache Kujifariji


Mchambuzi "Simba Wapatikane Wachezaji wa Maana Tuache Kujifariji"

Andiko la @jr_farhanjr kwenda kwa viongozi wa Simba SC

Timu ilipokuwa haifanyi vizuri Mashabiki wakapiga sana kelele, zilipozidi kelele wakaitwa Mashabiki wenye nguvu haswa mtandaoni yakaitwa maridhiano ya Viongozi na Mashabiki, ghafla upepo ukabadilika na timu ikaanza kupambwa, lakini ukweli unaopanda ngazi ukawa unaitazama tu timu, kilichopo sasa wala hakihitaji vikao ni UWEKEZAJI kifupi kikosi kinahitaji maboresho makubwa mno.

Kama vinahitajika vikao uitishwe Mkutano Mkuu wa dharura wa klabu na sio kundi flani kwakuwa hao sio Simba na hawawezi kuwa sauti ya Mashabiki wote, huku ni kuonana watoto! Hata Mkutano Mkuu unahitaji Wanachama, bahati mbaya Simba haina Wanachama wapya! Fanyeni kitu kimoja tumieni mitandao ya kijamii wekeni form kusanyeni maoni, jifungieni yapitieni vyema sana.

Tuachane na hizi Panadol na sindano za ganzi za sisi tupo vizuri kimataifa, mara ohoo Robo fainali tumefika sana, mara Mnyama kimataifa habari nyingine, tuachane kabisa na hizi historia! Tufanye kama hakuna kilichowahi kutokea, timu ianze upya! Wakati ni sasa sio kesho, tuachane na kujifariji fariji na matukio ndio yanatufelisha sana mpaka kesho.

Sasa muwe pia na Kamati ya usajili wekeni Wachezaji wa zamani, wekeni Makocha na wawepo Scouts wa maana Afrika ili wapatikane wachezaji wa maana, kazieni mifumo ya soka la Vijana ambalo mmelitelekeza, grassroots tutapata wakina Mkude na Ndemla wa maana tu pia wenye kufahamu utamaduni wa klabu, jaribuni kuimarisha mifumo tuachane na mambo ya mtandaoni kwanza.

Kocha kabla ya Robertinho alikuwa Zoran akaondoka zake, kaja Robertinho timu haikuwa inacheza vyema Mashabiki wakahoji Ikapigwa tano ghafla Robertinho hayupo! Bado timu inacheza vibaya na sasa anakuja Benchaki, kikosi ni kile kile? Tunatarajia miujiza? No thank you, UWEKEZAJI waletwe Wachezaji.

Tulipo sasa ni pazuri saaana ili klabu ianze upya, hatupaswi kufeli nusu nusu! Yaani tufeli kabisa ili tukubali kuanza upya kabisa! The new beginning is now Inawezekana mbona, mkiamua tu Viongozi! Wala hatuwafokei ila tunakumbushana tu.

Kama mdau una maoni gani ____?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.