Kocha Simba Anatakiwa Kufanyia Kazi Eneo la Kuruhusu Magoli - Ambangile
Mchambuzi wa soka Bongo, George Ambangile amesema, kwa kuwa eneo la kuzuia limeonekana kuwa na shida, Kocha wa Simba SC anatakiwa kufanyia kazi.
Ambangile amesema, anapaswa kukaa na wachezaji wake, kuwauliza kwanza wao ni nini kinasababisha waruhusu magoli kwenye mechi nyingi na wakifanyie kazi kuelekea mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, 2023 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
"Awaulize kwanza wao wenyewe lakini pia baada ya hapo awaoneshe video zao jinsi wanavyoruhusu na kupata suluhu ya pamoja," alisema Ambangile.