Kocha Mpya Simba Aweka Msimamo, Sinta Fagilia Urafiki wa Wachezaji na Mabossi
Kocha Mpya Simba Aweka Msimamo, Sinta Fagilia Urafiki wa Wachezaji na Mabossi

Kocha wa Simba wakati akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari, alisema hata angalia ukubwa au jina la mchezaji ili kumpa nafasi kwenye kikosi chake! Badala yake ataangalia wale wanaowajibika, kusikiliza na kutekeleza maelekezo kwenye uwanja wa mazoezi.


Kwa hiyo haijalishi mchezaji ana jina kiasi gani, ana umri mkubwa au mdogo, kama utafata kile ambacho anakitaka basi mtasafiri katika boti moja kuelekea kwenye kutekeleza malengo ya Simba.


Changamoto ambayo huwa inajitokeza mara nyingi ni wachezaji ambao wana urafiki na viongozi kwenye timu, akiona hapati nafasi kwa kocha anaenda kwa boss kulalamika kuwa kocha hampi nafasi ya kucheza.


Bosi anamwita kocha ofisini na kumwambia aangalie ni kwa namna gani mchezaji fulani anaweza kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake kutokana na umuhimu wa mchezaji huyo kwenye timu.


Hivyo ndio vitu ambavyo vinaleta changamoto kwa makocha. Kwa mfano, hivi karibuni mchezaji kama Shaban Chilunda na Abdallah Hamisi wamefanya mazoezi karibu wiki nzima lakini kuna wachezaji wengine hawakuwepo mazoezini kutokana na kuumwa, wamerudi mazoezini siku mbili kabla ya mechi na kwenye mechi wamepangwa!


Hii inawakata sana wachezaji ambao wanakomaa kwenye mazoezi halafu hawapati nafasi kwenye mechi, vitu kama hivi sitaki kuamini kama kocha anaefata taratibu anaweza kufanya mambo kama hayo ila ukifatilia utagundua kunakuwa na ushawishi wa watu fulani nyuma yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.