George Job: Simba inazidiwa ubora na Yanga

George Job: Simba inazidiwa ubora na Yanga


Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Wasafi FM Radio, George Job amesema kuwa Klabu ya Simba imezidiwa ubora na watani zao Yanga SC kwa misimu miwili mfululizo sasa.


Kauli hiyo ya Job inakuja baada ya Simba kukubali kichapo cha bao 5-1 kutoka kwa wapinzani wao hao.


"Hayo mengine ni matatizo madogo. Tatizo kubwa la Simba SC ni kutokukubali kwamba kwa sasa wamezidiwa ubora na Yanga"


"Ndio maana unaona (5) zinawachanganya wanatafuta mchawi lakini ukifuatilia katika misimu (2) iliyopita Yanga wamechukua makombe yote mbele ya Simba SC, hawajachukua kwa bahati mbaya ni Ubora wao uko juu ya Simba.


"Ni kama misimu (4) iliyopita, Simba walikuwa bora kuliko Yanga. Yanga wakakubali wakaboresha kikosi ukitazama kikosi cha Yanga hakuna mchezaji aliyesajiliwa mwaka 2020.


"Bila kukubali kuwa kwa sasa Simba wamezidiwa na Yanga wanapaswa kujipanga upya tatizo hilo haliwezi kuisha," amesema George Job.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.