Gamondi: Kwa Al Ahly sitarudia makosa ya CR Belouizdad

 

Gamondi: Kwa Al Ahly sitarudia makosa ya CR Belouizdad

 Gamondi: Kwa Al Ahly sitarudia makosa ya CR Belouizdad

Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Angel Gamondi amekiri wapinzani wao Al Ahly ya nchini Misri ni wagumu, lakini watawafunga watakapokutana Jumamosi (Desemba 02) kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es salaam.Timu hizo zitavaana katika mchezo wa Mzunguuko wa Pili wa Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa saa nne kamili usiku.


Young Africans wataingia uwanjani wakiwa wametoka katika hasira ya kufungwa mchezo wa kwanza michuano hiyo, dhidi ya CR Belouizdad ya nchini Algeria ambayo walishinda mabao 3-0.


Gamondi amesema kuwa hataki kurudia makosa aliyoyafanya katika mchezo uliopita, badala yake ataingia katika mchezo huo kivingine ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya ushindi dhidi ya Al Ahly.


Amesema kuwa wanatakutumia vema uwanja wa nyumbani katika mchezo huo, kwa ushindi utakaorejesha matumaini ya kufanya vema katika michezo ijayo watakayoicheza.


Ameongeza kuwa ana kibarua kigumu cha kuwandaa wachezaji wake, ili kupata matokeo mazuri ya ushindi nyumbani na hilo linawekana kwake kutokanana maandalizi makubwa anayoendelea kuyafanya kwenye kiwanja cha mazoezi.


“Siku zote kocha anajifunza kutokana na mchezo uliopita, hivyo binafsi kama kocha nimejifunza katika mchezo uliopita dhidi ya CR Belouizdad, na kufanya maboresho maboresho katika kila sehemu,”


“Kikubwa hatutaki kurudia makosa ambayo tumefanya katika mchezo dhidi ya CR Belouizdad, kuna makosa ya kiufundi tuliyafanya mimi na benchi langu, hivyo mashabiki waondoe hofu, kwani hayatajirudia tena tutakapokutana dhidi ya Al Ahly.


“Ninaamini ubora wa kikosi changu ambacho kinaundwa na wachezaji wenye uwezo na uzoefu wa kucheza michuano hii mikubwa ya kimataifa, hivyo hakuna kitakachoshindana,” amesema Gamondi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.