Alex Ngereza: Kuna wachezaji Simba wamepelekwa Kamati ya Nidhamu

Alex Ngereza: Kuna wachezaji Simba wamepelekwa Kamati ya Nidhamu

Wakati vuguvugu la mabadiliko likiendelea kuitafuna Simba baada ya kupokea kipigo kizito cha Bao 5-1 kutoka kwa Yanga Jumapili ya Novemba 5.


Kuna mengi yaliyosemwa kuhusiana na kipigo hicho huku ikitajwa kuwa kuna wachezaji walihusika kuihujumu Timu hiyo.


Sasa Mchambuzi wa Michezo kutoka TV3 anatudokeza kuwa tayari kuna wachezaji washafikishwa katika kamati ya Nidhamu ya Klabu hiyo iliyo chini ya aliekuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.


"Chama,Saido Ntibazonkiza na Hennock Inonga wamepelekwa kamati ya nidhamu baada ya kuhisiwa kwamba wali
husika kuihujumu Simba kwenye mchezo wa derby dhidi ya Yanga kwenye Ushindi wa magoli matano kwa moja"


Je unadhani ni kweli wachezaji hao walihusika kuihujumu mechi ya Mtani?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.