Timu ya SIMBA Watinga Makundi Kwa Mbinde, Goli la Ugenini Lawapa Faida

 

Timu ya SIMBA Watinga Makundi Kwa Mbinde, Goli la Ugenini Lawapa Faida

Timu ya SIMBA Watinga Makundi Kwa Mbinde, Goli la Ugenini Lawapa Faida

Wekundu wa Msimbazi Simba SC kwa mara nyingine katika Uwanja wa Chamazi Complex Jijini Dar es Salaam wanaonesha ukubwa wao wakikata tiketi ya kutinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba wanatinga hatua ya Makundi baada ya kulazimisha sare ya goli 1-1 na Power Dynamos ya Zambia na kupita kwa faida ya goli la ugenini baada ya kupata suluhu ya mabao 2-2 ugenini mwwzi uliopita.

Power Dynamos ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 16 ya mchezo kwa shuti kali la Andy Boyeli lililomshinda golikipa Ayoub Lakred.

Kipindi cha pili Simba walirudi kwa kasi na kufanya mabadiliko kadhaa na hatimaye dakika ya 68 John Bocco alipiga shuti lilomzidi beki wa Power Dynamos Kondwani Chiboni aliejikuta anawapa Simba goli la kusawazisha.

Mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo ya jumla ni 3-3 lakini Simba wakafanikiwa kusonga hatua inayofuata kwa faida ya goli la ugenini ambako walipata mabao mawili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.