Kiungo wa Azam, Yannick Bangala amerejea uwanjani baada ya kupona majeraha aliyoyapata Oktoba 3, mwaka huu kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji na huenda akacheza mechi ijayo dhidi ya Yanga, waajiri wake wa zamani huku kocha wa Azam akichekelea.
Bangala alichanika nyama za paja na kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili, lakini hivi sasa yuko tayari kucheza hivyo analisikilizia benchi la ufundi la timu hiyo kumpa nafasi.
Kocha mkuu wa Azam, Youssouph Dabo alisema “Tunafurahi amerejea, ataongeza kitu kwenye kikosi chetu kwani anauzoefu wa kutosha, Bado tunajiandaa na mechi ijayo, kumpanga au kutompanga itategemea ataonyesha nini hadi siku ya mwisho ya mazoezi. Tusubiri tutaona.”