Jezi feki za Yanga zanaswa Chang'ombe, GSM hasara ya bilioni 2

 

Jezi feki za Yanga zanaswa Chang'ombe, GSM hasara ya bilioni 2

Mwakilishi wa Kampuni ya GSM kwenye msako uliozikamata jezi feki za Simba, Yanga na Taifa Stars kwenye Ghala la Tosh Logistics lililopo Chang’ombe Dar es salaam amesema iwapo jezi hizo za Yanga pekee zingeingia sokoni zingeisababishia Kampuni hiyo hasara ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.


Ineshuhudiwa Maafisa wa Idara mbalimbali za Serikali usiku kucha kwenye Ghala hilo wakifanya tathmini ya mzigo huo ili kujua makadirio ya thamani yake halisi na hasara iliyopatikana pamoja na viwango na ubora wake huku Mmiliki wa mzigo huo akiwa hajaonekana kwenye eneo hilo toka ilipobainika.


Licha ya uwepo wa Maafisa wa Serikali, wengine waliokuwa katika eneo hilo hadi usiku mzito ni pamoja na Viongozi wa Simba na Yanga na Wawakilishi kutoka GSM na Sandaland ambao walionekana kufuatilia kwa ukaribu kila kilichoendelea.


Viongozi wa Taasisi za Serikali hawakuwa tayari kuongea huku wakiahidi kutoa taarifa zaidi baadae lakini Mwakilishi wa Kampuni ya GSM amesema kuwa uwepo wa jezi feki hizo unakwamisha jezi original kuuzwa.


Aidha, mwakilishi huyo mewataka Mashabiki kununua jezi halisi kwenye maduka yaliyotangazwa kwakuwa kunua jezi feki kunaua mpira wa Tanzania na kuwatia hasara wanaowekeza pesa zao kutengeneza na kusambaza jezi original.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.