Hakuna kiingilio kuwaona Mazembe kesho wakipepetana na Esperance

 

Hakuna kiingilio kuwaona Mazembe kesho wakipepetana na Esperance

TP Mazembe watacheza mchezo wao wa kwanza wa African Football League (AFL) katika dimba la Benjamin Mkapa dhidi ya Esperance De Tunis, mchezo huo hautakuwa na kiingilio na Mazoezi t imewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ikicheza dhidi ya watunisia.


TP Mazembe wamechagua kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa na inakuwa faida kwa Tanzania kushuhudia michezo mingine zaidi ya Africain Football League ambayo inasimamiwa na FIFA pamoja na CAF.


Mchezo kati ya Tp Mazembe dhidi ya Esperance hautakuwa na kiingilio na hivyo kila mtanzania na mpenda soka anaweza kwenda kesho Benjamin Mkapa kuwaunga mkono TP Mazembe.


Mazembe inawaomba mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuiongezea hamasa timu yao iliyouchagua kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.