HAJI Manara Yanga Bingwa LIGI ya Mabingwa Afrika Msimu Huu

 

HAJI Manara Yanga Bingwa LIGI ya Mabingwa Afrika Msimu Huu

Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema anaiona Yanga SC ikienda kushinda kikombe cha Klabu Bingwa Afrika msimu huu wa 2023/24.

Manara amesema kuwa amezitazama timu nyingi zilizofuzu hatua ya makundi ya Klabu Bingwa na kuona inawezekana kwa Yanga SC kushinda kikombe hicho.

“Yanga SC wana uwezo wa kuchukua hiki kikombe, wana timu imara ya kishindani katika kila idara, hivyo inawezekana kabisa wakachukua kikombe.

“Kama hawajawa mabingwa wajitahidi kufika hata hatua ya nusu fainali, lakini robo fainali ni hatua ambayo Simba SC huwa wanafika,“ amesema Haji Manara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.