Maxi Nzengeli Anabalaa Lake, Kiungo Huyu wa JKT Afunguka Jaramba Alilopigwa na Kijana Huyo Mdogo

 

Maxi Nzengeli Anabalaa Lake, Kiungo Huyu wa JKT Afunguka Jaramba Alilopigwa na Kijana Huyo Mdogo

Kiungo wa JKT Tanzania, Hassan Nassor Maulid ‘Machezo’ aliyesimama kati na kuchuana na Mudathir Yahya na Stephane Aziz Ki wa Young Africans katika mechi ya Ligi Kuu Bara na timu hiyo kupigwa mabao 5-0, amesema hakuna mchezaji aliyewanyimna raha kama Maxi Nzengeli aliyedai hakabiki uwanjani.

Timu hizo zilikutana mapema wiki hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Maxi akiendelea kutoa shoo ya maana akifunga mabao mawili na Machezo anasema licha ya kukabana na viungo wawili mahiri, Mudathir na Aziz KI, lakini aliyewatesa zxaidi ni Maxi.

“Mimi nilikuwa sina bato yoyote na Aziz Ki au Mudathir, nilichokuwa nafanya ni kutekeleza majukumu niliopewa na kocha, ila aliyetusumbua ni Maxi, kwani jamaa hakabiki kabisa,” amesema Machezo.

Amesema mara nyingi alikuvwa akijaribu kumkaba Maxi lakini hata ukimfanyia press unakuta keshatoa mpira mguuni kwake tofauti na wachezaji wengine

“Nikiri wazi kwamba aliyenipa tabu kwenye mchezo huo ni Maxi kwa sababu hata ukimfanyia press unakuta keshatoa mpira, ila kwa Aziz Ki nilimsoma vizuri alikuwa na chenga moja tu na Muda namuona wa kawaida, ndio maana namtaja aliyetusumbua, Maxi anajua sana,” amesema kiungo wa zamani wa Mbeya City.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.