Mastaa Yanga Wafunguka Siri ya Vipigo 'Hevi' Wanavyogawa "Shoo bado"

 

Mastaa Yanga Wafunguka Siri ya Vipigo 'Hevi' Wanavyogawa "Shoo bado"

Hakuna hofu tena kwa mashabiki wa Yanga, ambao mwanzoni walikuwa wanajiuliza kama watatoboa baada ya kuondoka watu muhimu kikosini, lakini sasa kocha mpya, Miguel Gamondi kaja kivingine akizidisha kicheko baada ya kuwa na hakika nyota yeyote wa timu hiyo anaweza kuwatungua wapinzani.


Sio kuwa na uwezo wa kufunga tu, bali nyota wa sasa wa Yanga ya Gamondi pia wanakaba kwa pamoja na kuwanyima nafasi kwa wachezaji wa timu pinzani kulifikia lango la timu hiyo kwenye mechi mbalimbali ilizocheza hadi sasa.


Ipo hivi. Japo vionjo na mbinu za ufundishaji vimekuwa tofauti, ila kicheki ni kilekile..


Yapo mambo yamebadilika kiufundi baada ya kusepa kwa Nabi, kocha Gamondi inaonekana timu yake ikicheza mastaa wakikaba na kushambulia kwa pamoja, jambo lilaowapa ugumku wapinzani, huku kila mchezaji anafunga.


Yanga imecheza mechi sita za mashindano na kufunga jumla ya mabao 18, huku maingizo mapya yakitisha kiuchezaji kwa timu inakaba kuanzia juu, ikinyang’anya mpira kutoka kwa wapinzani kwa haraka, huku ikifunga mabao yake kutoka kwenye maeneo mengi ya kikosi chao, kuanzia kwenye beki, viungo na washambuliaji.


Katika mechi sita Yanga imeruhusu bao moja tu la penalti, yenjye ikifunga mabao 18 yaliyochangiwa na wachezaji tisa.


Mazi Nzengeli anaongoza kifunga manne, akiafutiwa na Stephane Azizi KI mwenye matatu, huku Pacome Zouzoua, Hafiz Konkoni, Kennedy Musonda na Clement Mzize wana mawili mawili, wakati Dickson Job, Yao Kouassi na Mudathjir Yahya wana moja moja.


Akizungumza nasi Musonda alisema ubora wa Yanga unatokana na mfumo wa kocha pia ugeni wake unawapa chachu wachezaji kupambania namba.


“Ni kazi kwetu kuonyesha ili kujitengenezea uhakika wa kucheza ni kocha ambaye ametoa nafasi kwa kila mchezaji kumpa kile alichonacho hivyo ili kuendelea kujenga kikosi imara.” alisema MJusonda, huku Kibwana Shomari alisema ubora wa Yanga unachagizwa na wachezaji kupambania namba kwa vile kuna ingizo jipya la wachezaji

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.