Kanoute Hali Mbaya, Apumzishwe, Spirit ya Upambanaji Haipo

 

Kanoute Hali Mbaya, Apumzishwe, Spirit ya Upambanaji Haipo

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa wachezaji wengi wa Klabu ya Simba SC, wamechoka kwa sababu ya kutumika kwa muda mrefu bila kupumzika.

Wakanda amesema hayo akimtolea mfano Sadio Kanoute raia wa Mali kuw amechoka zaidi tofauti na kazi aliyokuwa kiifanya msimu uliopita ndani ya kikosi hicho.

“Mwalimu anahitajji utimamu wa wachezaji, mwalimu anahitaji utayari wa miili ya wachezaji, miili ya wachezaji wa Simba waliokuwepo msimu uliopita fatigue (uchovu) upo ndani ya miili yao, angalia work-rate aliyokuwa nayo Kanoute msimu uliopita halafu mwangalie Kanoute wa msimu huu.

“Huwezi kusema ni mchezaji mbovu lakini ile spirit ya upambanaji aliyokuwa nayo msimu uliopita na msimu huu unaona kabisa kuna namna imepungua, kwa sababu ni mchezaji ambaye amekuwa akitumika mfululizo kwa misimu karibia miwili mfululizo day in-day out unamuona Kanoute uwanjani,” Wakanda Republic.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.