Katika Maisha yake Bongo Fiston Mayele Hawezi Zisahau Timu Hizi Mbili, Alishindwa Kabisa Kutetema

Katika Maisha yake Bongo Fiston Mayele Hawezi Zisahau Timu Hizi Mbili, Alishindwa Kabisa Kutetema


Mshambuliaji mpya wa klabu ya Pyramids, Fiston Mayele atakumbukwa Yanga kwa ubora wake wa kupachika mabao na katika misimu miwili aliyokaa Jangwani amecheka na nyavu mara 33 kwenye Ligi Kuu katika misimu yake miwili.

Alianza na mabao 16 msimu wa kwanza na kukikosa kiatu cha dhahabu kilichokwenda kwa George Mpole aliyekuwa Geita Gold na kufunga mabao 17 na katika msimu wa pili alitupia mipira 17 nyavuni na kumaliza kinara akilingana na Saido Ntibazonkiza wa Simba.

Ila katika ubora huu mshambuliaji huyo aliyekuwa maarufu kwa staili yake ya kutetema hakuwahi zifunga timu za Simba na Ruvu Shooting katika mechi zote walizokutana misimu miwili.

Tanzania Prisons iliyokuwa katika listi ya Simba na Ruvu ilikubali kufungwa na Mayele katika mechi ya mwisho Ligi Kuu iliyopigwa Mbeya.

Mayele amewahi kuwatandika Simba katika mechi mbili za ngao ya Jamii lakini si katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.