Siri yafichuka Yanga walivyopiga chini dili la Ngoma

 

Siri yafichuka Yanga walivyopiga chini dili la Ngoma

Ni kweli kwamba uongozi wa Klabu ya Yanga walikuwa wanamhitaji Fabrice Ngoma raia wa Congo DR hapo awali tofauti na wapinzani wao, Simba Sc.


Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, klabu hiyo ilianza mazungumzo na meneja wa mchezaji huyo Faustino Mukandila lakini hawakufikia muafaka licha ya mazungumzo kufikia pazuri na dili likawa halina muendelezo kwa Yanga.


Simba wakawasiliana na meneja wa Fabrice Ngoma Kisha wakafanya mazungumzo wakitaka kumsajili,meneja akawataarifu Yanga kuhusiana na Simba kumtaka Ngoma, Yanga wao wakampa ruhusa meneja ya kupokea ofa.


Taarifa zinaeleza kuwa kiongozi wa juu wa Yanga aliwasiliana na Kocha Florence Ibenge juu ya kumsajili Ngoma Kisha akapewa ushauri ambao ameutekeleza juu ya usajili huo.


Majeruhi yanatajwa kuwa ni kikwazo cha nyota huyo ambaye amewahi kuitumikia RS Berkanechini ya Ibenge.


Hii inafanana na dili Kama ambalo lilikuwa kwa Simba na Eric Kabwe ambao walifikia hatua nzuri kwenye mazungumzo ya kumsajili lakini baadae hawakuwa na muendelezo mzuri Kisha akasajiliwa Uarabuni..


Hivyo Yanga hawajapokonywa mchezaji Airport ila ni mambo tu ya Simba na Yanga kama kawaida yao, ukipata nafasi mtambie mwenzako.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.