Juma Mgunda "Sadio Kanoute na Chama Hatutakuwa Nao"

Juma Mgunda "Sadio Kanoute na Chama Hatutakuwa Nao"


Kuelekea Mechi ya Ligi Kuu Ya NBC Simba Sc dhidi ya Polisi Tanzania kesho katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Kocha Msaidizi wa Simba Sc Juma Mgunda ameelezea maandalizi yao yalivyo mpaka sasa.

Mgunda ameesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo huku akitaja mastaa watakaoukosa mchezo huo.

"Maandalizi yote ya kucheza na timu nzuri ya Polisi hapo kesho yamekamilika. Huu ni mchezo muhimu wa Ligi na ni muhimu kwetu. Ilituonekane tumeshiriki vizuri ligi lazima tuucheze.

"Sisi tumejipanga kwa sababu tunajua ni muhimu ili kumaliza ligi vizuri. Ni mechi ambayo ina umhimu wa kipekee.

"Wachezaji ambao tutawakosa ni Chama kwa sababu ana adhabu ya TFF ya kutocheza mechi tatu za ligi, pia tutamkosa Sadio Kanoute ambaye naye ana kadi tatu za njano na ameondoka kikosini yupo nchini kwao, waliobaki wote wapo tayari kuitumikia Simba kesho," amesema Mgunda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad