Feisal Salum na Eng. Hersi Wakisaini Mkataba |
FeisalSalum amesema "Nilikaa kwa Saa sita na Kiongozi wangu wa Yanga, alikuwa yeye na Makamu wake, nikamwambia waliyokuwa wakinitendea, akasema tusameheane, nikamwambia nimemsamehe lakini siwezi kubaki"
Akihojiwa na CloudsFM ameongeza "Shida yangu #Yanga ni manyanyaso si mshahara, nilisaini Mkataba wa Miaka miwili kumbe yeye Kiongozi aliongeza Mwaka mmoja bila ridhaa yangu, mkataba uliandikwa kwa Kiingereza"
Amesisitiza, "Fedha ya usajili tulikubaliana Tsh. Milioni 100 kwa pamoja, pia si kweli walinipa Fedha yote, nilipomaliza kusaini mkataba waliniingizia Tsh. Milioni 10 tofauti na tulivyokubaliana, ikaenda hivyo kupewa hela mpaka tugombane ndio wananipa kimafungumafungu"