Yanga Kutangazwa Bingwa Ligi Kuu Leo?

Published from Blogger Prime Android App

Leo ni mwendelezo tena wa Ligi Kuu ya NBC zikipigwa mechi mbili kwenye viwanja viwili tofauti [GEITA GOLD V/s MBEYA CITY na YANGA V/s DODOMA JIJI.

Mbeya City ikiwa ugenini [Geita] itakuwa kwneye vita ya kuhakikisha inapata alama tatu ili kuondoka kwenye eneo la kucheza play offs ili kubaki Ligi Kuu.

Hadi sasa Mbeya City ina alama 27, ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi, endapo itashinda mchezo wa leo itafikisha alama 30 na kusogea hadi nafasi ya 12.

Geita Gold yenyewe ipo nafasi ya tano na alama zake 37, haiwezi tena kumaliza ndani ya top four hata ikitokea Singida Big Stars ikapoteza mechi zote zilizobaki.

Mechi ya usiku [YANGA V/s DODOMA JIJI] ni nafasi kwa Yanga kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu 2022|23 endapo itashinda mchezo wake dhidi ya Dodoma Jiji.

Endapo Yanga itashinda mchezo, itafikisha alama 74 ambazo haziwezi kufikiwa na Simba ambao ndio washindani wake kwenye mbio za ubingwa hadi sasa.

Simba ina alama 67, ikishinda mechi zake mbili zilizosalia itafikisha alama 73. Kwa maana hiyo ushindi wa Yanga leo dhidi ya Dodoma Jiji utahitimisha mbio za Simba kuwania ubingwa wa Ligi Kuu.

Dodoma Jiji watatibua sherehe za Yanga? Ikiwa Dodoma Jiji wataizuia Yanga kupata alama tatu, watakuwa wamekwamisha sherehe za Yanga kutangaza ubingwa wao wa 29 wa Ligi.

Dodoma Jiji ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 31, eneo ambalo sio salama kwao [Dodoma Jiji] kwa sababu alama zao zinaweza kufikiwa/kupitwa na Mtibwa Sugar na Mbeya City ambazo zipo kwenye hatari ya kucheza play offs.

RATIBA | LIGI KUU

⚽️ GEITA GOLD V/s MBEYA CITY
🏟 Nyankumbu Stadium, Geita
⌚️ Saa 8:00 Jioni

⚽️ YANGA V/s DODOMA JIJI
🏟 Azam Complex, Dar
⌚️ 10:00 Jioni

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.