Yanga Chali Yapigwa Chini Ligi Hii...Mwana FA Awaombea Ushiriki...Sakata Zima Liko Hivi

Yanga Chali Yapigwa Chini Ligi Hii...Mwana FA Awaombea Ushiriki...Sakata Zima Liko Hivi


Yanga Chali Yapigwa Chini Ligi Hii...Mwana FA Awaombea Ushiriki...Sakata Zima Liko Hivi

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mohamed Mwinjuma amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Veron Mosengo- Omba.


Katika mkutano huo ulifanyika Aprili 7, 2023 Durban nchini Afrika Kusini, Mwinjuma ametumia fursa hiyo kwa niaba ya Serikali kuiomba CAF iangalie namna itakavyoiwezesha Tanzania


ikishirikiana na Kenya na Uganda kuandaa mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa pamoja.


Amesema hatua hiyo inatokana na mashindano hayo kutowahi kufanyika katika ukanda wa Afrika Mashariki.


Aidha Mwinjuma amewasilisha ombi la Serikali la kuwa mwenyeji katika upangaji wa timu (droo) ya mashindano ya Super League pamoja na kuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza mwezi Novemba, 2023 na kama ikitokea nafasi ya kuongeza timu basi CAF iipatie kipaumbele timu ya Yanga.


Katika mazungumzo hayo Mwinjuma pia amefikisha salaam za shukrani za Serikali ya Tanzania kwa CAF kukubali kuufanyia marekebisho Uwanja Benjamin Mkapa baada ya timu ya Simba kuchaguliwa kushiriki mashindano ya Super League.


Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa (CAF), Veron Mosengo-Omba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoutoa kwa maendeleo ya mpira wa miguu Barani Afrika akamhakikishia Naibu Waziri, Mwinjuma kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania.


Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na utayari wa kuandaa mashindano ya AFCON ya Mwaka 2027 kwa pamoja na nchi za Uganda na Kenya.


Ametoa wito kwa nchi za Afrika Mashariki ziwasilishe maombi mapema kwa kuwa mashindano ya Super Cup hayajawahi kufanyika katika ukanda wa Afrika Mashariki akibainisha kuwa maombi yameanza kupokelewa kuanzia Aprili 5, 2023 na yanatarajiwa kufungwa baada ya siku 21.


Kuhusu kuiongeza timu ya Yanga katika mashindano ya Super League Katibu wa CAF amemueleza Mhe. Mwinjuma kuwa kwa sasa wamechukua timu chache lakini baadaye Tanzania itaingiza timu mbili ambazo ni Simba na Yanga.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.