Usajili wa Mayele Kwenda Vipers ya Uganda Gumzo Nchini Humo, Yanga Watamwachia?

Mayele


​Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers, Alex Isabirye ametolea ufafanuzi juu ya timu hiyo kuhusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele.


Akizungumza kutoka Kampala Uganda, Isabirye amesema hakuna kocha asiyependa kufanya kazi na mchezaji kama Mayele kutokana na ubora alionao kwenye mashindano ya ndani na nje lakini sio jambo rahisi kihivyo na hawana pumzi ya kumng’oa kwenye klabu yake ya sasa Young Africans.


“Kwa sasa ni nani ambaye hajui ubora wa Mayele? binafsi sidhani hata klabu yake iko tayari kumuacha mchezaji kama yeye kwenye kikosi chao kutokana na alivyoisaidia na kuipa mafanikio hadikufika hapa ilipo,” amesema.


Kwa upande wa kocha wa zamani wa Simba SC, Moses Basena amesema ni ngumu kwa timu za Uganda kutunushiana misuli na timu za Tanzania kutokana na kutokuwa na hali nzuri za kiuchumi kwani wamekuwa wakiwekeza kwa vijana wadogo.


“Najua vizuri timu za hapa (Uganda) kifedha zimeyumba sana sasa kusema wamtoe Mayele Young Africans kuja hapa kwangu naona kama miujiza kwa sababu hawatoweza kumlipa maana hata wanaocheza huku wanatamani kuja huko Tanzania.”


Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uganda, vimeripoti timu hiyo kumuhitaji Mayele huku vikinukuliwa Vipers SC imeweka ofa mezani ambayo ni kati ya Dola za Marekani 50,000 (Shll7milioni) hadi Dola 100,000 (Sh230 milioni).


Habari za uhakika zinasema kwamba wachezaji wengi wa Vipers wanalipwa kati ya Tsh.500, 000 mpaka 1500,000 huku Mayele kwa sasa akikadiriwa kuvuka 10 Milioni kwa mwezi.


Hivyo mitandao inamaanisha kwamba anaweza kulipa hata nusu ya timu kwa mwezi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad