Tajiri Huyu Akitua Tu United, Usajili Wa Kwanza Ni Mbappe

Mbappe

SHEIKH Jassim anataka kumsajili Kylian Mbappe iwapo atainunua Manchester United kwa kitita cha pauni bilioni 5, huku nyota wa Bayern Munich na Real Madrid wakiwemo kwenye orodha yake.

Sheikh Jassim anaongoza kundi la Qatar linalotaka kuchukua mikoba ya kuimiliki Manchester United na tayari nyota kama Kingsley Coman na Eduardo Camavinga pia wanaripotiwa kulengwa kwenye mipango ya kuwanunua.

Jassim anashindana na Sir Jim Ratcliffe kununua United kutoka familia ya Glazers.

Sheikh Jassim anataka kumnunua Kylian Mbappe kutoka Paris Saint-Germain mara tu atakapokamilisha mchakato wa kuinunua Manchester United.

Yeye ni mmoja wa vyama viwili vinavyofikiriwa kuwa miongoni mwa wagombea wakubwa pamoja na Sir Jim Ratcliffe wanaposhindana kununua hisa kubwa ya Old Trafford kutoka kwa familia ya Glazer.

Hata hivyo Mbappe amesaini mkataba na PSG hadi msimu wa joto wa 2024.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.