Bodi ya Ligi imeupangia tarehe mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa baada ya mchezo dhidi ya Malumo Gallants
Mchezo huo utapigwa May 13 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Yanga inahitaji kushinda mchezo huu ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu
Aidha mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS utapigwa May 21 katika uwanja wa LITI, Singida
Mchezo huo utapigwa siku nne baada ya mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Malumo Gallants