Simba Watupwa nje Kombe la Azam Sports, Azam Wafuta Uteja Kibabe

Simba Watupwa nje Kombe la Azam Sports, Azam Wafuta Uteja Kibabe

Dakika 90 zinakamilika katika Uwanja wa Nanganda Sijaona Mkoani Mtwara huku zikishuhudia vigogo Simba SC wakitupwa nje ya michuano ya Azam Sports Federation.

Mchezo huo wa Nusu Fainali ulizikutanisha Timu za Dar es Salaam Simba dhidi ya Azam FC na kumalizika kwa Azam kutinga hatua ya Fainali baada ya ushindi wa bao 2-1.

Azam ndio waliokuwa wa kwanza kubata bao kupitia kwa Lusajo Mwaikenda dakika ya 22 baada ya Mlinda mlango kushindwa kuudhibiti mpira wa adhabu uliopigwa na Lyanga.

Haikuwachukuwa Simba muda mrefu kusawazisha bao kwani dakika ya 28, Kiungo Sadio Kanoute aliwarudisha Simba mchezoni kwa bao la kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Said Ntibazonkiza.

Alikuwa ni Prince Dube alieingia kutokea benchi ambae ndie alikuja kuwapa Azam uhakika wa kuelekea kwenye Fainali mkwakwani baada ya kupachika bao la pili kwa Azam na mpaka Dakika 90 zinatamatika Azam wakaibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Azam anasubiri mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya Singida Big Stars dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga.

Mchezo wa Fainali ya Kombe la Azam Sports Federation utapigwa katika Uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga.

Hii ni mara ya kwanza Azam kuiondosha Yanga katika hatua ya mtoano ya Kombe la Azam Sports kwani hapo awali walishakutana mara mbili na Azam kupoteza mara zote.Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.