Mwanasheria wa Yanga Afunguka Tena Sakata la Fei Toto Baada ya Kukwama Tena "Aje Tuongee"

 
Mwanasheria wa Yanga Afunguka Tena Sakata la Fei Toto Baada ya Kukwama Tena "Aje Tuongee"

Mwanasheria wa Yanga Afunguka Tena Sakata la Fei Toto Baada ya Kukwama Tena "Aje Tuongee"


Anaandika Wakili Msomi @simon.esq, Mkurugenzi wa sheria wa @yangasc.


Kwa ridhaa ya Yanga (klabu ya Wananchi) napenda kuongelea kwa mara ya mwisho sakata la mdogo wetu Feisal Salum na kilichotokea jana;


Mdogo wetu kwa mara nyingine tena aliandika barua kutaka kuvunja mkataba na klabu ya Yanga akaipeleka TFF akiwataka wao ndio wavunje mkataba.


Sisi kama klabu tuliitwa TFF na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, ambacho ni chombo chenye hadhi ya kimahakama. Yanga tuliweka mapingamizi manne kuhusu maombi ya Feisal;


1. Shauri linalohusu uvunjifu wa mkataba “Contract termination“ lilishasikilizwa na kutolewa maamuzi na kamati kwenye maamuzi ya kwanza na maamuzi ya rejea (review). Hivyo kamati ileile haiwezi kusikiliza shauri lilelile na kwa muktadha uleule (Res judicata).


2. Kwakuwa suala hili limeshasikilizwa na kutolewa maamuzi hapo awali, hivyo mikono ya kamati imeshafungwa na sheria (Functus officio).


3. Kwa kuwa mikono ya kamati imeshafungwa, hivyo basi Kamati haina tena mamlaka (Jurisdiction) ya kusikiliza suala hili. (The committee lacks any power to re-examine decision).


4. Mkataba unaotaka kuvunjwa ni kati ya Yanga na Feisal, wao ndio wenye uwezo wa kuuvunja, na sio TFF kwa sababu TFF sio wahusika wa mkataba huo. Kisheria inaitwa "Privity of Contract" yani huwezi kuvunja mkataba ambao wewe sio sehemu yake.


Hivyo basi TFF hawana mamlaka yoyote kisheria kuvunja mkataba wakati wahusika wa mkataba, hawajakaa kwa ajili ya kuvunja mkataba wakashindwana.


Hoja hujibiwa kwa hoja (argumentum per argumentum). Mambo ya sijui mimi namwakilisha Drogba hayatuhusu. Hata kama ungekuwa unamwakilisha Messi na Ronaldo, dakika 10 ni nyingi sana kujibu hoja.


Mwisho; Feisal ni mdogo wetu na ni ndugu yetu. Anakaribishwa muda wowote kuja Yanga kuleta maombi ya kuvunja mkataba na atapewa baraka zote na klabu. Na huu ndio msimamo rasmi wa Yanga.


Jumaa Mubarak 🙏🏿


#Myatake:

Nimefurahi kuona Yanga wako tayari kumalizana na Fei. Ni jambo la kiungwana. Zile "vuta nikuvute" hazikuisaidia Yanga wala Fei. Yanga inaweza kusonga bila Fei, na Fei anaweza kusonga bila Yanga. Amalizane na Yanga, apate klabu anayoipenda, atumikie kipaji chake. Thats win win situation.!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad