Marumo Gallants Wapinzani wa Yanga Mdebwedo, Wachapwa 2-0 na Mamelodi

Marumo Gallants vs Mamelodi
Marumo Gallants vs Mamelodi

Klabu ya Marumo Gallants wakiwa nyumbani kwao katika Dimba la Peter Mokaba wamekubali kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa wababe wa soka la Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini umepigwa jana Jumamosi huku mabao ya Mamelodi yakifungwa na Thapelo James Morena dakika ya kwanza na Themba Zwane dakika ya 52. Wakati huo huo Mamelodi wakiongoza kwa umiliki wa mpira kwa asilimia 62 dhidi ya 38 za Marumo.

Kwa matokeo hayo, Marumo wapo nafasi ya tatu kutoka mwisho (nafasi ya 14) wakiwa na alama 29 katika michezo 29 waliocheza wakati Mamelodi wakiwa kileleni na alama 69.

Marumo ambao ni wapinzani wa Yanga katika hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika wanatarajiwa kucheza na miamba hao wa soka Tanzania Jumatano, Mei 10, 2023 katika Dimba la Mkapa na kurudiana Mei 17, nchini Afrik Kusini kusaka tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo.

Matokeo ya jana ya Marumo ni faida kwa Yanga kisaikolojia kwani wapinzani wao wametoka kufungwa nyumbani, wapo kwenye hatihati ya kushuka daraja na wanakwenda kucheza michuano mikubwa Afrika tena ugenini lakini Yanga wanapaswa kuchanga karata zao vizuri kwani soka lina matokeo yasiyotarajiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.