DONE DEAL | Tayari @wacofficiel imemtambulisha rasmi aliyewahi kuwa Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck kuwa Kocha wao Mkuu.
Januari 2021 Sven aliondoka Simba na kujiunga na AS FAR Rabat ya Morocco ambayo kwa kipindi kifupi aliipa mafanikio makubwa!
Aliiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu nyuma ya vigogo Wydad Casablanca na Raja Casablanca katika misimu miwili mfululizo.
Mafanikio makubwa zaidi kwake kwenye soka la Morocco ni kuchukua ubingwa wa kombe la mfalme na kutangazwa Kocha bora wa msimu 2020|21.
Kwa hiyo Sven si Kocha mgeni nchini Morocco.