Lionel Messi Aandaliwa Ofa Ya Kufuru Na Serikali Ya Saudia

 

Lionel Messi Aandaliwa Ofa Ya Kufuru Na Serikali Ya Saudia

SERIKALI ya Saudi Arabia imeandaa ofa kubwa zaidi katika historia ya soka lao ili kumnasa Lionel Messi.


Matajiri hao wanataka kutengeneza historia mpya kwenye ligi ya Saudia, wakitaka kuwa na miamba miwili ya soka duniani, ikiwemo Cristiano Ronaldo anayecheza Al-Nassr FC.


PSG, huenda ikawa bila Messi msimu ujao baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kutofanyika hadi sasa, huku tetesi zikidai PSG ina mpango wa kupunguza mastaa kwenye timu yao.
Kama dili la Messi litatiki basi anaweza kulipwa pauni milioni 320 kila mwaka, karibu mara mbili ya pauni milioni 165 anazolipwa Ronaldo.


Fowadi huyo anatarajiwa kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu, huku baba yake, Jorge, akiripotiwa kuiarifu klabu hiyo ya Ufaransa kuhusu uamuzi huo mwezi mmoja uliopita.


Klabu ya Al Hilal ndiyo inatajwa kwenye mpango huu wa kumchukua Messi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.