Kuhusu Ishu ya Kipa Manula wa Simba Kuwa NJE Msimu Mzima, Ukweli Halisi Ndio Huu

 

Golikipa wa Simba SC, Aishi Manula
Kipa Manula wa Simba

Kipa namba moja wa Simba SC, Aishi Salum Manula atakosekana kwenye michezo iliyosalia katika mashindano yote mpaka mwisho wa msimu huu.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally wakati akizungumza na wanahabari mjini Mtwara ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya Kombe la shirikisho dhidi ya Azam FC.

“Nyota wetu wote wapo vizuri na timamu ila mchezaji ambaye bado ni majeruhi ni Aishi Manula ambaye yeye kuna uwezekano mkubwa akakosekana hadi mwisho wa msimu, lakini vilevile Mohammed Ouattara naye bado anasumbuliwa na majeraha”

“Lakini nyota wengine wote simba tupo nao hapa rwangwa na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa nusu fainali dhidi ya Azam FC,” amesema Ahemd Ally.

Simba sasa wamelazimika kuanza kumpa mazoezi kipa namba nne Ahmad Feruz ili kusaidiana na kipa namba tatu, Ally Salim baada ya Beno Kakolanya kuwa na changamoto ya kimkataba na klabu yake huku akihusishwa kusaini Singida Big Stars.

Manula anasumbuliwa na tatizo la nyonga mabapo mpaka sasa amekosa mechi sita mpaka sasa kutokana na tatizo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.