Kama kweli tunampenda Feisal Salum basi kwasasa walipaswa kuwa wameshafika FIFA kwa ajili ya hili sakata lake dhidi ya Yanga, kwakuwa CAS ni mfumo wa kimahakama changamoto yake ni MUDA na GHARAMA za kesi, hivyo wanaweza kwenda FIFA.
Wengine tunaoonekana hatumpendi Feisal ila kiuhalisia sisi tunampenda sana na tunahitaji sana Maestro arejee uwanjani kuendelea na soka lake! Jana nilipata wasaa wa kuongea na Wanasheria kadhaa na watu wa mpira.
Ibara ya 54 ya FIFA inasema kitu kuhusu Football Tribunal ambapo migogoro kama hii ina maeneo yake na utatuzi wake! Football Tribunal ina chemba tatu nazo ni Dispute Resolution Chamber, Player Status Chamber na Agents Chamber! Hapo Feisal angeenda tu kwenye Dispute Resolution Chamber (DRC).
Wanasheria wake wangefile suala lake (ground) kisha wangeomba nafasi kwa FIFA wamruhusu Kijana aendelee kucheza mpira kwenye timu yoyote wakati suala lake linaendelea kusikilizwa kwakuwa ni miezi mitano sasa yupo nje.
Nimepata mfano wa kesi kama ya Feisal! Ambayo imepishana kwenye vitu vidogo tu! Kwenye suala la Feisal ni rahisi sana kwakuwa maswali yangekuwa machache sana ndio maana hata Mwanasheria wake alipewa dakika 10 tu za maelezo.
FIFA kupitia DRC wangepitia vitu vichache sana kama ifuatavyo!
Mchezaji ana mkataba na Yanga? NDIO! Amevunja mkataba wake? NDIO! Sababu za kuvunja mkataba, ni just cause ama without just cause? Jibu ni Without Just cause (bila sababu maalum)! Amevunja muda gani? Wakati msimu unaendelea! HAPA NDIPO KUNA KOSA.
DRC wangeendelea! Ametumikia mkataba wake kwa muda gani? Amevuka nusu ya mkataba! Maana yake yupo kipindi gani? Yupo Unprotected period (ambapo) atapaswa kulipa faini bila adhabu ya kufungiwa.
DRC wangekuja kutazama tena kwenye malipo ya mkataba! Unilateral termination inasemaje? Anapaswa kulipa Million 100 na mishahara ya miezi mitatu! Je amebakiza muda gani kwenye mkataba? Inapigwa hesabu kisha inatajwa faini ya Kijana kulipa.
Mpeni ushauri sahihi Kijana, TAFADHALINI, wakati Feisal amekubali kugeuzwa content anapaswa atambue hatua sahihi za kupita! Yanga wametaka mkamalizane kwakuwa ndicho FIFA wataenda kukifanya hicho hicho, chagua busara usipoteze muda.