Chelsea yajiondoa vita ya Victor Osimhen
Klabu ya Chelsea imesitisha mazungumzo na SSC Napoli kuhusu dili la Mshambuliaji wa klabu hiyo ya mjini Naples, Italia Victor Osimhen kwa sababu inaona ni vigumu kumpata katika usajili wa majira ya Kiangazi.
Chelsea inataka kusubiri hadi katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani ambapo mkataba wa Osimhen utakuwa umebakisha mwaka mmoja.
Mshambuliaji huyo kutoka nchini Nigeria msimu huu amecheza mechi 35 za michuano yote na kupachika mabao 28.
Man Utd mdogo mdogo kwa Lautaro Martinez
Baada ya Chelsea kusimamisha mazungumzo ya dili hilo inazipa nafasi timu za Manchester United, FC Barcelona na PSG ambazo zimeonyesha nia ya kumnasa mwishoni mwa msimu huu.
PSG inaenda kuachana na Lionel Messi inataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji na inaamini Osimhen ni chaguo sahihi. Wakati huo huo Barca ina matumaini ikimsajili Messi basi itakuwa imeongeza ushawishi wa kumchukua straika huyo pia.