CAF yatoa tamko hili kuhusu taa kuzimika uwanja wa Taifa

Taa Uwanja wa Taita


Ripoti ya Kamati maalumu ya CAF ya kukagua miundombinu ya viwanja kwa ajili ya Maandalizi ya Michuano ya CAF Super Leagu imesema kuwa taa zinazotakiwa kwenye Uwanja wa Mkapa ni lazima ziendane na utaratibu wa CAF.Imeeleza Taa za kiwango cha chini zinazotakiwa ziwe na Lux 1200 kuzunguka uwanja mzima ambazo kwa sasa kwa Mkapa hazijafungwa, hivyo ni jambo linalotakiwa kabla ya michuano hiyo, pia lazima kuwe na jenereta la dharura ambalo linaweza kufanya kazi wakati linapotakiwa.


Taarifa hiyo imeonyesha kuna mfumo pia mbovu kwenye uwekaji wa taa hizo ambao wanaona unatakiwa kuwekwa upya ili kukidhi kutumika kwa michezo ya usiku. Marekebisho hayo yanatakiwa kufanyika kwa wiki sita hadi nane kuanzia Mei 15 mwaka huu.


Taa za uwanja huo hasa eneo la kuchezea zimekuwa zikizima mara kadhaa wakati wa mechi (Mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda, Yanga dhidi ya Rivers United) jambo linalosababisha mechi kusimama kwa muda mrefu.Ikumbukwe pia kuwa, CAF imeshaagiza uwanja huo kufanyiwa maboresho makubwa kwa ajili ya kujiandaa ya michuano ya Africa Super League itakayoanza kutimka vumbi mwezo Agosti 2023.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.