Azam Chochoro la Simba Kuchukua Kombe la Azam Federation...Historia Itajirudia Leo?

Published from Blogger Prime Android App


Mtwara | Wakati Simba inachua ubingwa wa Azam Sports Federation Cup mara mbili mfululizo [2019|20 na 2020|21] iliitoa Azam FC kwenye hatua za Robo Fainali na Nusu Fainali.

Julai 2020 Simba iliifunga Azam FC kwa magoli 2-0 kwenye mchezo wa Robo Fainali uliocheza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Magoli ya Simba yalifungwa na John Bocco na Clatous Chama.

Simba ikaenda Nusu Fainali na kukutana na Yanga, Mnyama akampa Mwananchi 4-1 na kwenda Fainali ambapo alicheza na Namungo FC na kubeba Kombe la ASFC.

Juni 2021 Simba ilikutana tena na Azam FC kwenye mchezo wa Nusu Fainali na kushinda mchezo huo 1-0. Goli pekee kwenye mchezo huo lilifungwa na Luis Miquissone.

Simba ikaenda Fainali na kutwaa tena taji hilo baada ya kuifunga Yanga 1-0 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Leo Azam FC inakutana tena Simba kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Je, Simba itaendeleza ubabe kwa Azam au Azam watakataa uteja?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.