Amri Kiemba "Njia Walizopita Congo Kimpira Ndio Nasisi Tunapita Huko Sasa"

Published from Blogger Prime Android App

Njia ambazo zimepita klabu za DR Congo na sisi ni kama tunapita hukohuko, tumewekeza sana kwenye vikosi kwa ajili ya kushindana lakini klabu bado zipo vilevile.

Yani ndani ya uwanja klabu zetu zinaonekana kukua lakini nje ya uwanja bado mambo ni yaleyale. Mfano kama klabu ilikuwa haina ‘training facilities’, haiwezi kuzalisha wachezaji wengine bado mambo yamebaki hivyohivyo.

Kwa hiyo wanachofanya ni kusajili, hii ni njia mojawapo ya kujitangaza na kujiinua lakini huwa ni ya muda mfupi kwa sababu hakuna misingi na hiki ndicho wanachopia wenzetu wa DR Congo.

Wachezaji mahiri wa DR Congo wote wanaondoka lakini miaka ya nyuma wakati uwekezaji ni mkubwa walikuwa wanabaki palepale kwao. Sasa hivi klabu nyingine zinachukua wachezaji kutoka AS Vita na Mazembe.

Hapa katikati uchumi wa klabu za DR Congo uliyumba zikawa haziwezi tena kukaa na wachezaji wenye thamani kubwa matokeo yake zikageuka kuwa klabu za kuuza wachezaji kwenda klabu zenye misuli ya kiuchumi.

Ukiangalia klabu za Tanzania huoni kama kuna njia ya kuzalisha wachezaji wengine wala kutengeneza misuli ya kiuchumi ukiachana na hisani ya watu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.