Ahmed Ally Afunguka Machungu "Tumezomewa kutoka Mtwara hadi Dar"

Ahmed Ally Afunguka Machungu "Tumezomewa kutoka Mtwara hadi Dar"

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amezungumza kwa masikitiko kuhusiana na hali wanayokumbana nayo wachezaji na viongozi wa timu hiyo baada ya kushindwa kupambania taji lolote msimu huu.


Simba jana ilitolewa kwenye Kombe la Azam Shirikisho ikifungwa mabao 2-1 na kuaga michuano hiyo ambayo iliweka matumaini baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali na Wydad Casablanca huku Ligi Kuu matumaini yakiwa madogo.


Ahmed kupitia ukurasa wa Instagram ameandika haya; "Mara kadhaa utasikia shabiki anasema sisi tunaumia kuliko wachezaji au viongozi. Ndugu zangu ili mradi sote tuna damu ya Simba basi wote tunapitia maumivu, kinachotokea ni tofauti ya mtu na mtu kuhimili maumivu."


"Ndiyo maana wengine wanalia, wengine wanazimia, wengine wanashindwa kula, wengine wanakasirika yote ni maumivu. Leo tumezomewa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaaam hali ambayo inawaumiza zaidi wachezaji, hakuna mchezaji anayetaka kufungwa makusudi ili azomewe kuzomewa ni kitendo cha aibu sana."


"Katika nyakati hizi ni vema kila mmojaakaheshimu maumivu ya mwenzie kwani hakuna anaejua mwenzie anaumia kiasi gani. Tufanye yote lakini tuwaache viongozi wamalize kuugulia baada ya hapo waje watutengenezee timu madhubuti kwa ajili ya msimu ujao. Hakuna mtu anaekubali kuharibikiwa katika kazi yake, viongozi wetu wanapambana usiku na mchana kuhakikisha sisi mashabiki tunapata furaha."


"Tuwaunge mkono kwenye kipindi hiki kigumu kwao kwani na wao wanaumia kama sisi na hawana mahala pa kupeleka lawama zao, lakini pia pamoja na kuumia kwao wanatakiwa warudi kazini kututengenezea Simba imara,"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.